March 8, 2020

BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji wa Yanga leo ametenda kazi yake iliyomleta Bongo kwa kuifunga Simba bao 1-0 kwenye mchezo wa mzunguko wa pili uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Bao pekee la ushindi lilifungwa dakika ya 44 kwa mpira wa adhabu alioupiga kiungo huyo raia wa Ghana na kuuzamisha mazima langoni baada ya Aishi Manula kuzidiwa nguvu na mpira huo.

Mpaka dakika 90 zinakamilka Simba ya Meddie Kagere ilishindwa kufurukuta mbele ya Yanga waliokuwa wakifanya mashambulizi ya hatari huku nyota wa mchezo kwa Yanga akiwa ni Metacha Mnata ambaye aliokoa michomo mingi ya hatari kwa Simba iliyokuwa ikipigwa na Meddie Kagere.

Ushindi wa leo unaifanya Yanga kufikisha pointi 50 ikiwa imecheza mechi 25 huku Simba ikiwa na pointi 68 imecheza mechi 27 za Ligi Kuu Bara

6 COMMENTS:

  1. Simba hakuna muda wa kupoteza. Tujifunze tulipoteleza. Tuko vizuri kwenye ligi na Federation cup. Majeruhi wawahi kurudi ratiba bado ni tight sana. Michuano ya CHAN nayo hii hapa na CAF champions league inaanza Agosti. Hakuna muda wa kupoteza.

    ReplyDelete
  2. Wachazeji wazee wasiponunuliwa mechi hawana chochote. Mmedhibitiwa ujanja ujanja wenu safari hii

    ReplyDelete
  3. Wanayanga Bhana, Simba wamewaacha kwa 18 points , hata mkishinda viporo vyote baado mko mbali sana, msikamie Simba jipange , simba inaenda kuchukua kombe mara ya 3 mfululizo hamuoni kuna haja ya kuangalia namna ya ushangiliaji huu ?

    ReplyDelete
  4. Wana Simba kuna haja ya kuwatafakari viongozi wenu waliotaka eti msije uwanjani kuipa support timu yenu kisa Yanga watapata pesa nyingi. Hii ni ushaidi wapo clubuni pale kimaslai na sio mapenzi ya timu. Wapo radhi timu ifungwe kwa kuwa hawana mgao.

    ReplyDelete
  5. Maneno ya faraja sana kwa Mikia ila poleni sana Mikia wote. Nadhani wengine mmeanza kushabikia mpira hv karibuni.Yanga kuchukua mara 3 mfululizo walishazoea sasa ni marudio tu. Mjipange bila kuja na matokeo kutoka home

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic