UONGOZI wa Yanga umesema kuwa leo unaichapa Simba mapema ili kulinda heshima hauna hesabu na kutwaa Kombe la Ligi Kuu Bara ambalo lipo mkononi mwa Simba.
Leo Uwanja wa Taifa majira ya saa 11:00 jioni, Yanga itakuwa mwenyeji wa Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao utakuwa ni wa pili kwao kukutana msimu huu ule wa kwanza Simba ililazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2.
Antonio Nugaz, Ofisa Uhamasishaji wa Yanga amesema kuwa kichapo kwa Simba hakiepukiki kutokana na maandalizi ambayo wameyafanya kwa muda mrefu.
"Tumefanya maandalizi kwa muda mrefu, itakuwa furaha kwetu kuifunga Simba ili kuweka heshima, wao hata wakitwaa ubingwa sisi kazi yetu ya kwanza itakuwa imekamilika hakuna kitakachotukwamisha.
"Mashabiki mjitokeze kwa wingi Uwanja wa Taifa, tumekuwa na mwitikio mzuri na matokeo bora hivi sasa tupo vizuri ni lazima tushinde," amesema.
Duh hatar
ReplyDeleteHa ha ha ha ha.
ReplyDeleteWanakubali ubingwa hawaupati na leo watachapwa
ReplyDeleteRudia huo msemo leo,mikia mnaamin kwenye giza mwanga upo Yanga
DeleteHivi mpira ni saa 11 na siyo 12 tena waoendwa nsije kupitwa
ReplyDelete