MEDDIE
Kagere mshambuliaji kinara wa utupiaji wa Simba na kiungo Francis Kahata
wameonyesha balaa kwa kutupia na kutengeneza nafasi za mabao na kuitikisa idadi
ya mabao ya Yanga waliyonayo kwa sasa ndani ya Ligi Kuu Bara.
Yanga ambao
watakuwa wenyeji kwenye mchezo wa leo dhidi ya Simba utakaopigwa Uwanja wa
Taifa, wametupia jumla ya mabao 29 kwenye mechi 24 walizocheza huku Simba
wakitupia mabao 55.
Kagere na Kahata pacha yao imehusika kwenye mabao 30.
Kagere
ametupia mabao 15 na kutengeneza nafasi 5 za mabao, Kahata ametupia mabao manne
na kutengeneza nafasi sita za mabao ambapo moja ya bao la Kahata alimpa Kagere
Uwanja wa Taifa mbele ya Azam FC kwenye ushindi wa bao 1-0.
Luc Eymael,
Kocha Mkuu wa Yanga yeye ngao yake kubwa ni David Molinga ambaye ni mtaalamu wa
kutupia akiwa na mabao nane kwa Yanga na Patrick Sibomana mwenye mabao matano kwa sasa.
Eymael amesema: "Wapinzani wetu natambua wana kasi kubwa ya kufunga na wametuzidi pointi ila haina maana kwamba itatuogopesha hapana tunatafuta mbinu za kupata ushindi.
0 COMMENTS:
Post a Comment