March 23, 2020

IMEELEZWA kuwa mshambuliaji mzawa namba moja ndani ya Namungo FC, Reliants Lusajo amewekwa kwenye rada na mabosi wa Yanga ili kuinasa saini yake kwa ajili ya kujiunga na kikosi hicho.

Lusajo ndani ya ligi ametupia mabao 11 na kutengeneza pasi nne za mabao ambapo anamfukizia kwa ukaribu mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere mwenye mabao 19 kwa kucheka na nyavu.

Habari zinaeleza kuwa Yanga imeweka hesabu za kumpata nyota huyo kuwa mbadala wa kutatua ubutu wa safu yao ya ushambuliaji ambayo kwa ujumla kwenye mechi 27 imefunga mabao 31 huku kinara wa kutupia akiwa ni David Molinga mwenye mabao nane.


Meneja wa Lusajo, Ahmad Kassim amesema kuwa suala la mchezaji wake kusepa ndani ya Namungo ni la muda tu kwani amebakiza kandarasi ya miezi mitatu jambo linalompa nafasi ya kuzungumza na timu yoyote.

"Kwa sasa Lusajo yupo huru kuzungumza na timu yoyote ana  mkataba wa miezi mitatu ndio umebaki kuhusu kwenda Yanga ni suala la kusubiri kwani mazungumzo bado hayajafanyika ila kipaumbele kikubwa ni kwa Namungo," amesema.

1 COMMENTS:

  1. Kama hamuwezi kuuweka siri mkija kutolewa tonge kinywani na wenye hela yanguvu msije kusema mnaonewa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic