March 23, 2020


KIPRE Tchetche, nyota wa zamani wa Azam FC anayekipiga Klabu ya Kedah inayoshiriki Ligi Kuu ya Malaysia amewekwa kwenye rada za Simba ilikuongeza nguvu ya Kikosi hicho.

Msimu wa 2011 mpaka 2016 nyota huyo alikipiga ndani ya Azam FC anafamiana vema na nahodha wa Simba John Bocco ambaye kwa wakati huo alikuwa akikipiga ndani ya Azam FC.

Habari zinaeleza kuwa uongozi wa Simba umeanza kufanya mazungumzo na wachezaji wa kimataifa ili kupata huduma zao.

Mshambuliaji huyo anakumbukwa kwa kutumia nguvu nyingi na akili ndani ya Uwanja ambapo msimu wa 2013/14 walitwaa taji la Ligi Kuu Bara bila kupoteza mechi. 


"Tchetche anahitajika ndani ya Simba ila mkwanja wake ni mrefu na anataka mshahara wa dola 8,000 kwa mwezi hapo ndipo tatizo lilipo,". Ilieleza taarifa hiyo.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa amesema kuwa kwa sasa hawezi sema chochote mpaka muda wa usajili ukifika.

3 COMMENTS:

  1. Endeleeni kutusajilia ili muuze magazeti

    ReplyDelete
  2. Mmeanza tena kuleta magasa yenu ili mpige hela michezaji mizee ya nini

    ReplyDelete
  3. Mmeanza kuokota wachezaji ambao hawana lolote lile ili mumpige pesa MO? Nimeamini hapo simba wamewekwa wapigaji ili watuharibie timu yetu tu hiyo kazi ni kocha achaguwe yeye sio hao wapigaji wasio na uchungu na timu yetu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic