April 19, 2020

UONGOZI wa Azam FC  leo unakumbuka miaka sita iliyopita baada ya kutwaa Kombe la Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza bila kucpoteza mchezo.

 Aprili 19, 2014 Azam FC iliweka alama yao kwenye vitabu vya kumbukumbu vya soka hapa nchini pale ilipomaliza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kwa kutwaa taji hilo kwa mara ya kwanza.

Ilikuwa katika mchezo dhidi ya JKT Ruvu Stars (sasa JKT Tanzania) ambapo ilishinda 1-0, kwa bao la dakika ya 78 lililofungwa na straika kutoka nchini Uganda, Brian Umony.

Mechi hii ilipigwa baada ya wiki moja baada ya kutwaa ubingwa pale ilipoifunga 2-1 Mbeya City jijini Mbeya, kwa mabao ya Gaudence Mwaikimba na nahodha John Bocco ambaye kwa sasa anakipiga ndani ya Klabu ya Simba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic