WACHEZAJI wa
Arsenal, wamekubali kukatwa asilimia 12.5 ya mishahara yao, baada ya kuahidiwa bonasi
kubwa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Wachezaji hao
watafidia fedha watakazokatwa kwa kila mmoja kulipwa pauni laki moja endapo
watafuzu kucheza Ligi ya Mabingwa ya Ulaya msimu ujao.
Klabu pia,
imeahidi kumlipa kila mchezaji bonasi ya pauni laki tano (Sh bilioni 1.4) kama watatwaa taji la Ligi
ya Mabingwa Ulaya mwaka 2021 au pauni laki moja (Sh milioni 287.9) kama wataibuka mabingwa wa Europa
League.
Endapo Arsenal
itafuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao wa 2020/21, inamaanisha
kwamba wachezaji wa timu hiyo fedha zao zinazokatwa hivi sasa zitarudi zote.
Arsenal,
imekuwa klabu ya kwanza ya Ligi Kuu England, kukubali mpango wa kukata
mishahara kwa wachezaji wake, katika kipindi hiki ambacho klabu nyingi duniani
zimeathirika kiuchumi kutokana na janga la Virusi vya Corona.
0 COMMENTS:
Post a Comment