Kipa wa Real Madrid, Thibaut Courtois hivi karibuni katika siku ya kimataifa ya makipa aliwashukuru makipa wakongwe Casillas na Van der Sar ambao nidiyo alikuwa anawafuatilia zaidi.
Courtois kwa sasa ni mmoja wa makipa bora Ulaya kutokana na kazi ambayo amekuwa akifanya ndani ya Madrid msimu huu, licha ya kwa sasa ligi kusimama.
Katika makuzi yake mpaka anacheza soka kipa huyo wa Madrid alikuwa anawafuatailia zaidi makipa hao kama role mode wake kwenye soka.
Siku ya kimataifa ya magolikipa ilifanyika hivi karibuni, lakini ilipoa kutokana na hali ya sasa ya dunia ya Virusi vya Corona.
Courtois kupitia mtandao wake wa kijamii aliweka picha yake akiwa mdogo huku akiwashukuru Casillas na Van der Sar kwa kila ambacho alijifunza kupitia wao.
Kipa huyo alisema: “Shukrani na saluti kwa makipa wenzangu wote katika siku hii muhimu ya kimataifa kwa makipa.
“Lakini pongeza na shukurani zangu kwa Casillas na Van der Sar kwa kuwa ndiyo ambao nimekuwa nikiwaangalia tangu mdogo.
“Nawashukuru sana hawa wamekuwa na mchango mkubwa kwangu na kunifanya kuwa bora mpaka hapa nilipofika sasa,” alisema kipa huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment