April 17, 2020

SENZO Mazingisa,Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba amesema kuwa timu yake haishindwi kumsajili mchezaji yeyote anayecheza katika ligi ya Tanzania ikiwa inamhitaji.

Simba imekuwa ikihusishwa na usajili wa baadhi ya wachezaji wanaocheza Ligi Kuu Bara kama beki wa Coastal Union, Bakari Mwamnyeto, beki wa Azam FC, Yakubu Mohammed na kiungo wa Polisi Tanzania, Baraka Majogoro. 

Senzo amesema kuwa kutokana na aina ya wachezaji wanaopatikana hapa nchini, timu hiyo haishindwi kumsajili mchezaji yeyote ambaye watakuwa wakimhitaji labda kama hawana mpango na mchezaji huyo.


"Ikiwa tunahitaji kupata saini ya mchezaji ndani ya Ligi Kuu Bara Tanzania hatuwezi kushindwa labda tuwe hatuna mpango naye," amesema.

1 COMMENTS:

  1. Kabisa hakuna ubishi juu ya hilo Profesa Masimgiza na hata hao mawakala kama kweli wana wachezaji wanaoamini kuwa wana uwezo watakuwa hawawatkii future njema ya baadae wachezaji wao kwa kujali pesa peke yake kwa kuwapeleka timu ambazo hazina malengo ya kimataifa bila ya kujali makuzi ya mchezaji husika siku zijazo. Hata kama mimi ningekuwa ni mchezaji mwenye malengo basi kwa Tanzania ningeipa simba nafasi ya kwanza na sababu sio pesa tu bali simba ya sasa imejengwa kwa ajili ya kushiriki mashindano ya kimmataifa mvua inyeshe au isinyeshe hayo ndio malengo ya simba na uwezo huo wanao na kunako mechi za kimataifa ndio kunako mtoa mchezaji ingawa bado vijana wetu wa kitanzania hawajaamka katika hili kwani kunahitaji jihadi na kujitoa misili ya injini za ndege inapoanza kupaa angani unapopata nafasi ya kimataifa kuonyesha uwezo wako ili uonekane kwani ushindani ni mkubwa kwenye soko la ajira ya mpira.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic