April 15, 2020


UONGOZI wa Simba umesema kuwa ishu ya nyota wao Clatous Chama kuibukia ndani ya Yanga haiwezi kutokea kutokana na kulipwa mshahara mrefu ambao hawezi kulipwa Yanga.

Chama ambaye ni raia wa Zambia amekuwa na mchango mkubwa ndani ya Simba akiwa ametoa pasi saba za mabao na amefunga mabao mawili pia.

Kumekuwa na mvutano mkubwa wa mabosi wa Yanga na Simba ambao kila upande unavutia kwake ambapo Yanga wanahitaji saini yake huku akiwa ni mali ya Simba kwa sasa.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema:"Hatuwezi kumuachia mchezaji wetu ambaye tunamtaka kwenda kwa wapinzani wetu ilhali tuna mkataba naye lakini kwa sasa hawezi kwenda kwa jirani hawana uwezo wa kumlipa mshahara.

"Ni jambo lisilowezekana kwa Chama kuondoka Simba kwenda Yanga, bado tunamhitaji na mkataba wake ni mpaka 2021, ikiwa wanamhitaji ni lazima wafuate utaratibu," amesema.

3 COMMENTS:

  1. Yaani tumechoka huku ndani korona tukitoka nje mambo ya malumbano,jamaani hebu mwacheni mwenyewe aamue

    ReplyDelete
  2. Kuchamba kwingi huondoka na uchafu badala kuusafisha na ngoma ikilia Sana haichelewi kuchanika na mbio za sakafuni huishia ukingoni, hayo waliyatamka wa kale.

    ReplyDelete
  3. Kama zuzu Manara anasema Yanga hawawezi kumlipa mshahara Chama,sasa kwanini analia eti wataenda kuwashtaki Yanga TFF kwa kuongea nae?"Jicho" kubwa uume kwa jirani!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic