KOCHA Mkuu wa Tanzania Prisons, Adolf Rishard amesema kuwa ili mchezaji adumu kwenye ubora wake ni lazima awe na nidhamu ndani ya uwanja na nje ya uwanja kwa kuzingatia kanuni za afya.
Adolf amesema kuwa wachezaji wanapaswa wawe makini katika kila jambo ambalo wanafanya ili kulinda uwezo wao kwa muda mrefu.
"Ni kitu cha msingi kwa mchezaji kuwa na nidhamu ndani ya uwanja na nje ya uwanja kwa kuzingatia kile ambacho anakula pamoja na kunywa jambo litakalompa uhai katika maisha ya soka.
"Ulevi hautakiwi kwa wachezaji kwani wanatakiwa kuwa makini na kile wanachokiingiza ili wazidi kulinda vipaji vyao, kwa kipindi hiki kigumu cha Virusi vya Corona ni muhimu kuwa makini," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment