SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba ameweka wazi kuwa anahitaji viungo wakali wenye uwezo mithili ya Luis Miqussone ambao anaamini watampa matokeo ndani ya uwanja.
Miqussone ambaye ni kiungo wa Simba kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona alianza kuingia kwenye mfumo wa Sven kutokana na kubadili matokeo akiwa ndani ya uwanja licha ya kutumia dakika chache.
Tayari Mbelgiji huyo ametoa mapendekezo yake ya aina ya wachezaji anaowataka huku akisisitiza kwamba anahitaji viungo wenye uwezo wa kunyumbulika zaidi kama ilivyo kwa Miqussone.
Akiwa amejiunga na Simba kwenye dirisha dogo la msimu huu mwezi Januari Miqussone alicheza mechi 8 na alifunga mabao matatu na kutoa pasi moja ya bao lililofungwa na Meddie Kagere kwenye mchezo dhidi ya Bashara United na ametumia dakika 624 uwanjani.
Mechi zake hizi hapa:-JKT Tanzania (90), Mtibwa Sugar (16), Kagera Sugar (90), Biashara United (90), KMC (75) na Azam (83), Yanga (90), Singida United (90)
0 COMMENTS:
Post a Comment