May 25, 2020


MIKAEL Silvestre, nyota wa zamani ndani ya Klabu ya Manchester United amefichua kuwa David Beckham aliwahi kupigwa na kiatu usoni na bosi wao Sir Alex Ferguson kwa kile alichodai kuwa alikuwa chanzo cha kuipoteza timu.

Tukio hilo lilitokea Old Trafford mwaka 2003 baada ya United kukubali kichapo mbele ya Arsenal kwenye mchezo wa FA raundi ya tano.

Mikael amesema kuwa Ferguson alikasirishwa na kitendo cha kupigwa chini kwenye mashindano ya FA mapema ilihali walikuwa na nafasi ya kushinda.


 "Nilikuwepo wakati haya yanatokea, kila mmoja alishtuka lakini ni vitu ambavyo huwa vinatokea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.

 "Lilikuwa ni shuti ambalo lilipigwa na bosi ila ilikuwa bahati mbaya kiatu kikakutana na uso wa Beckham na kumpasua karibu na eneo la jicho. 

"Alikuwa ni mwenye hasira hakuna aliyeweza kumzuia hilo halikuisha kwenye mioyo yao ndio maana msimu unaofuata Beckham aliibukia Real Madrid," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic