May 25, 2020


LAWRENCE Mwalusako, mchezaji wa zamani wa Klabu ya Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars miaka ya 1998 amefariki leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipewa matibabu.

Mbali ya kufanya vizuri ndani ya uwanja, aliwahi kuwa kiongozi ndani ya Yanga ambapo alikuwa Katibu Mkuu mwaka 2012 enzi za uhai wake.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema ni pigo kwa Taifa kwani alikuwa ni mtu wa michezo.


 "Ni pigo kwa watu wa michezo wote sio Yanga pekee, alijitoa kwa moyo katika kazi na Taifa pia, tunaendelea kutoa ushirikiano kwa familia," amesema.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa msiba upo Kimara nyumbani kwa marehemu alipokuwa akiishi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic