FEISAL Salum, kiungo anayekipiga ndani ya Klabu ya Yanga amesema kuwa katika maisha yake ya soka aliwahi kusepa timu yake ya Aston Villa na kutua Klabu ya Calypso kwa kupewa viatu vya kuchezea mpira.
Fei amesema kuwa timu zote hizo ni za kitaa kwao Visiwani Zanzibar ambapo alikuwa akicheza kabla ya kutua Yanga.
"Nilikuwa nakipiga Aston Villa nikasajiliwa na Calypso zote za Zanzibar, walinipa viatu nami nikaanza kukipiga kwenye timu mpya.
"Kabla ya hapo nilikuwa ninanunua viatu mwenyewe ama shabiki akielewa kazi yangu ananinunulia licha ya kuwa nilikuwa mdogo nilikuwa ninagombaniwa na timu nyingine," amesema.
Fei Toto kwa sasa yupo Zanzibar baada ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa kutokana na janga la Virusi vya Corona.
Duu yaani wewe kweli debetupu
ReplyDeleteNi rahisi Sana kumfahamu mwenzio
ReplyDeleteChenga ww
ReplyDelete