MWADUI FC ya Shinyanga ipo nafasi ya 12 kwenye msimamo ikiwa na pointi zake 34 kibindoni.
Imecheza mechi 28 ambazo ni dakika 2,520 imeshinda mechi nane huku ikipoteza mechi 10 ambazo ni sawa na idadi ya mechi ilizolazimisha sare.
Imetupia kimiani mabao 27 ikiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 93 na kufungwa mabao 32 ikiwa na wastani wa kufungwa bao kila baada ya dakika 78.
Aishi Manula mlinda mlango wa Simba hajasahau lile bao la kichwa alilotunguliwa na Gerald Mdamu wa Mwadui FC lililotaka kumtegua nyonga.
Mchezo huo Simba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0.
Ujinga tu.Hiyo kampeni ya kipumbavu ya kutafuta timu zilizoifunga Simba haziwezi kupunguza gepu ya pointi 21.
ReplyDeleteKila siku wekeni stori mpya. Tunangoja ya JKT nae si alimfunga Simba.
Nakubaliana na mwandishi wa hapo juu.Ingekuwa ni timu fulani inaongoza ligi kwa pointi 20 na kimetokea balaa hili la COVID 19 basi zingeandikwa makala nyingi tu ili timu hiyo upele ubingwa. Kwa sababu sio chaguo lao kimyaaa lakini huwezi kuziba jua kwa ungo. Jua litachomoza na bingwa anayestahili atapewa ubingwa wake.
ReplyDelete