May 6, 2020


IBRAHIM Ajibu, kiungo mshambuliaji wa Simba amesema kuwa dili lake la kutua Simba aliwashirikisha ndugu zake pamoja na nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta anayekipiga Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu England.

Ajibu alikuwa na ofa mbili mkononi msimu wa 2018/19 alipokuwa Yanga ambapo TP Mazembe nao walikuwa wanahitaji saini yake pamoja na Simba.

Yote hayo yalitokana na mchango wake mkubwa ndani ya Klabu ya Yanga ambapo alikuwa ni mtengeneza mipango akiwa  na pasi 17 za mabao na alitupia mabao sita.

Ajibu amesema:"Niliwashirikisha ndugu zangu ambao ni familia yangu pamoja na Samatta ambaye aliniambia kuwa hawezi kunichagulia timu zaidi ya kunisharuri nitazame timu itakayonipa furaha."

Kwa sasa Ajibu yupo ndani ya Simba ambapo alisaini kandarasi ya miaka miwili na inaelezwa dau lake lilikuwa ni milioni 80.

4 COMMENTS:

  1. Na anafuraha sana kuwepo benchini kuchoma mihogo

    ReplyDelete
    Replies
    1. jamaa punguza ukali wa maneno.
      unajua wachezaji wengi wa hapa kwetu hata hawana uwezo wa kuchanganua mambo. Jibu na gadiel walianza kuwa na majina makubwa sana nadani ya Tz, na Yanga ndio iliwafanya kuwa na majina hayo, sawa mpira ni popote, Ajibu anapata diliTp Mazembe anaona kuwa kutokana na kidada chake cha kutaka kucheza na Mashabiki hawez kupata kampani kule kwa wanaotaka kazi ya maana. anaamua kubaki simba kwa mil. 80 ambazo angezipata hata akiwa yanga hasa kwa kiwango na mchango aliouonesha.
      najiuliza ajibu angekuwaje kwa huu ujio wa morison? nafikiri angekuwa tishio zaid. muone masikin Gadier michael, na Kakolanya,
      hawakujifunza kwa D.Dida kwa alivyosota alipokuwa simba.
      hawajifunzi kwa Yondan alivyo na msimamo

      Delete
    2. Huna chochote cha kushauri maana maamuzi ni yao, mbona Terry aligoma kwenda kucheza timu za ligi kuu na akaenda timu za Championiship? kila binadamu anayoyake hata wewe hapo mapungufu ni mengi mno sema tu hawakwambii yawezekana hao unawasema tayari ni maarufu wanajulikana hivi unajua kuna timu 20 na kila timu inawachezaji kuanzia 25? jiulize je ni hao tu ndo wako benchi? heshimu maamuzi ya binadamu wenzako usiwadharau wala kuwadhihaki kwa mawazo yao'

      Delete
    3. Kama navyokuona pale Tandale Uzuri magengeni unavyo furahia kuuza vipande vya papa na nguru.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic