May 7, 2020


 JUSTIN Shonga,mshambuliaji wa kimataia wa Zambia ni miongoni mwa wachezaji ghali sokoni hivyo kibongobongo kuvunja benki ili kuipata saini yake lazima ukae.

Mzambia huyo amekuwa akihusishwa kutakiwa na Simba tangu msimu uliopita wakati ilipokuwa nchini ya Mbelgiji, Patrick Aussems kabla ya kusepa na kwa sasa mikoba yake ipo kwa Sven Vandenbroeck.


Mbelgiji wa sasa wa Simba, Sven amewahi kuwa kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Zambia ‘Chipochipolo’. 

Kwa mujibu wa jarida la Kickoff kutoka nchini Afrika Kusini, Mzambia huyo ni miongoni mwa wachezaji kumi wenye thamani kubwa katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini, akiwa na thamani ya euro 600,000 sawa Sh bilioni 1.5 za Kitanzania.

1 COMMENTS:

  1. Mufilisi huyo aende tu.labda kama akipata mpira hapokonywi mpaka afunge,SIMBA kwakuwashauri tu achaneni na huyo jamaa kabisa ataharibu kila kitu bajeti kubwa itakwenda kwa mchezaji mmoja alafu itakuaje?ina maana hatusajili wengine acheni ujinga bhana.alafu ni mchezaji wa kawaida sana kwa sasa yani ameshuka kiwango,fanyeni scouting bhana acheni kubeba magarasa yaliyochokwa na wengine.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic