KIUNGO wa Atalanta
ya Italia, Andrea Rinaldi, amefariki dunia akiwa na miaka 19 baada ya mishipa
yake ya damu katika ubongo kukumbwa na tatizo.
Tatizo hilo
lilimpata Ijumaa iliyopita wakati akifanya mazoezi binafsi nyumbani kwake kipindi
hiki ambacho kuna katazo la kuepuka mikusanyiko kutokana na uwepo wa corona.
Baada ya
kukaa hospitali kwa takribani siku tatu, jana Jumatatu alifariki dunia.
Rinaldi amekulia
katika timu ya vijana ya Atalanta na mpaka anafikwa na umauti, alikuwa akiichezea
Legnano kwa mkopo ikiwa ni timu inayoshiriki Serie D. Alicheza mechi 23 na
kufunga bao moja msimu huu.
Kiungo huyo
alikuwa na Atalanta iliyopo Serie A tangu akiwa na miaka 13, ameshinda Kombe la
Ligi la vijana chini ya miaka 17 na Super Cup mwaka 2016.








0 COMMENTS:
Post a Comment