May 12, 2020


AMIS Tambwe, raia wa Burundi mshambuliaji wa zamani wa Yanga amesema kuwa anatamani kurudi kukipiga  ndani ya klabu hiyo.

Tambwe alijiunga na Yanga msimu wa 2014/15 baada ya kupigwa chini na Simba aliachwa na Yanga msimu wa 2018/19 na alitimka mpaka Oman ila kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba na klabu yake hiyo.

Tambwe amesema:"Miongoni mwa timu ambazo zimenipa heshima ni Yanga sina cha kuwalipa zaidi ya kufanya nao kazi tena kwa mafanikio mengine.

 "Nikipata nafasi ya kurudi nitafurahi na nitafanya kazi kwa juhudi ninapenda kuwa pale mpaka nitakapostaafu maisha yangu ya  soka."

 Msimu aliosepa Tambwe alitupia mabao 12 ambapo 8 alifunga kwenye ligi na manne alifunga kwenye Kombe la Shirikisho.

2 COMMENTS:

  1. Ukiona kimya baada ya kuonesha mapenzi yako, ujuwe kuwa ndio Hawana haja nawe tena na Hakuna haja ya kuendelea kujizalilisha. Jamaa wanataka damu mpya

    ReplyDelete
    Replies
    1. Dah nimechekaa kama ni mazuri.Kwani Tambwe umesahau nini Yanga?Tambwe umri au uwezo umepungua?kama ni umri mbona kina Kagere,Yondani,Nyoni mnalingana kiumri?Kama unajiamini kuwa uwezo unao na unapenda kucheza ligi ya Tanzania basi ni kheri utafute timu zingine kama KMC,Namungo n.k.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic