JADON Sancho, amezidi kuwa bora ndani ya Klabu yake ya Borussia Dortumund jambo ambalo linaifanya Manchester United kuzidi kupasua kichwa kuinasa saini yake.
Sancho ametupia jumla ya mabao 14 huku akitengeneza nafasi 15 za mabao ndani ya klabu yake hiyo.
Anaingia anga za Lionel Messi kuwa mshambuliaji aliyefunga mabao zaidi ya 10 na kutoa pia pasi zaidi ya 10.
Miongoni mwa timu ambazo zinaiwinda saini yake kwa udi na uvumba ni pamoja na Chelsea, Liverpool, Manchester City ambayo ni klabu yake ya zamani.








0 COMMENTS:
Post a Comment