KOREA Kusini
jana Ijumaa iliruhusu ligi yao kuanza kuchezwa ambapo Jeonbuk Hyundai Motors FC
iliifunga Suwon Bluewings FC bao 1-0.
Katika mchezo
huo wa kwanza, ulishuhudiwa ukichezwa bila ya mashabiki huku kukiwa na baadhi
ya sheria mpya zikiwekwa.
Sheria hizo
ni; Hakuna kutema mate, chupa za maji za wachezaji zina majina, waandishi wa
habari kukaa mita mbili katika chumba cha mikutano, wachezaji na watu wote wa
benchi la ufundi kupimwa kwanza afya zao.
Baada ya
mchezo huo mmoja wa jana, leo Jumamosi zimechezwa mechi singing tatu ambapo
matokeo yake ni; Gwangju FC 0-2 Seongnam, Incheon 0-0 Daegu na Ulsan Hyundai 4-0
Sangju Sangmu.
Wachezaji na
viongozi wa benchi la ufundi walionekana kuvaa barakoa.
Ikumbukwe kuwa,
baada ya kuwepo kwa mlipuko wa virusi vya corona, ligi mbalimbali duniani
zilisimama na zingine kuahirishwa kabisa.
Hivi karibuni,
kumekuwa na matumaini ya ligi kurejea tena ambapo Mei 16, mwaka huu, Bundesliga
inatarajiwa kuendelea, kisha La Liga, Premier na Serie A nazo kuna uwezekano
zikaendelea Juni, mwaka huu.










0 COMMENTS:
Post a Comment