LIONEL Messi, staa wa Barcelona, amesema kuwa wana kikosi bora ila wanatakiwa kubadili aina ya uchezaji wao bila kufanya hivyo hawawezi kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Barcelona kwa sasa kwa upande wa Ligi ya Mabingwa Ulaya wapo hatua ya 16 na mchezo wa mwisho walicheza na Napoli na kutoa sare ya 1-1 kwenye La Liga ni vinara na pointi zao 58.
Barca inaonekana kuyumba hata kufikia hatua ya kumfukuza aliyekuwa Kocha Mkuu Ernesto Valverde na nafasi yake ikichukuliwa na Quique Setien.
"Sina wasiwasi na kikosi chetu tunaweza kushinda kila kilicho mbele yetu lakini si aina ya uchezaji wetu wa sasa tuatakiwa kubadilika,".
0 COMMENTS:
Post a Comment