May 26, 2020


INAELEZWA kuwa uongozi wa Yanga upo kwenye hesabu za kuboresha kikosi chake msimu ujao ili kuleta ushindani kwenye mechi za ligi na mashindano mengine.

Tayari kwa sasa kuna majina ambayo yanatajwa kuwa kwenye hesabu za mabosi hao wa Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu Luc Eymael.

 Wanaotajwa kuwa kwenye rada za Yanga kwa sasa hawa hapa:-Relliats Lusajo wa Namungo, Bigirimana Blaise wa Namungo hawa ni washambuliaji huku kiungo Luka Kikoti naye akiwa kwenye orodha.

Bakari Mwamnyeto na pacha wake Ibrahim Ame mabeki wa Coastal Union, Baraka Majogoro wa Polisi Tanzania, Yassin Mohamed wa Polisi Tanzania.
Yusuph Mhilu wa Kagera Sugar ni mshambuliaji.

2 COMMENTS:

  1. Yanajirejea hayo kwa hayo ni upuuzi mtupu

    ReplyDelete
  2. Wenye timu wameshakanusha na wanasema hawapo tayari kuwatoa au mnawataka wachukuliwe kwa maguvu wakimtaka wasitake

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic