May 27, 2020


WACHEZAJI wa Simba leo baada ya kuwasili kambini wamefanyiwa vipimo vya afya ambavyo ni muhimu kwa ajili ya kuelekea maandalizi ya kumaliza mechi za mzunguko wa pili.

Akizungumza na Saleh Jembe, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa kwa sasa wapo kambini ikiwa ni maandalizi ya kuelekea kwenye mechi za ligi pamoja na Kombe la Shirikisho.

'Tumeshawasili kambini na wachezaji wameanza kuripoti, kikubwa ambacho kinafanyika ni kuanza kuwafanyia vipimo ili kujua afya zao kisha program nyingine zitafuata,"

Miongoni mwa wachezaji ambao wamewasili kambini leo ni pamoja na nahodha msaidizi Mohamed Hussein, Shomari Kapombe, Beno Kakolanya na Said Ndemla.

1 COMMENTS:

  1. Salejembe punguzeni ushabiki kwa Simba na Yanga toeni habari zilizo fair kwa vilabu vyote mfano Mwadui, Namungo, JKT Tanzania siwasikii

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic