TIMU ya Alliance FC, leo inamenyana na Klabu ya Namungo kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa leo Uwanja wa Majaliwa majira ya saa 10:00 huku ushindani ukitarajiwa kuwa mkubwa.
Alliance FC inayonolewa na Kocha Mkuu Kessy Mzirai inakutana na mpinzani wake Namungo iliyo chini ya Kocha Mkuu, Hitimana Thiery.
Hatua hii ya robo fainali mshindi atakayeshinda atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Sahare All Stars na Ndanda FC.
Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho ataiwakilisha nchi kwenye michuao ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho.
Bingwa mtetezi wa taji hilo ni Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Aristica Cioaba.
0 COMMENTS:
Post a Comment