IKIWA kesho wanakutana kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali, Uongozi wa Simba umepanga kikosi kazi cha Azam FC ambacho ni hatari kikiwa uwanjani.
Simba itamenyana na Azam FC Uwanja wa Taifa majira ya saa 1:00 usiku.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara kupitia Ukurasa wake wa Instagram amewapanga namna hii huku akisema kuwa hajatazama wale ambao wapo nje ya nchi kutokana na 'loc down':-Razack Abarola amemuweka langoni.
Agrey Morris amesema kama ana miaka 20 hivi
Yakub Mohamed
Mudhathir Yahaya amesema ni mpiganaji uwanjani
Salum Abubakar, 'Sure Boy' amesema ni mpiga pasi bora.
Idd Kipagwile
Idd Naldo mtihani mkubwa
Obrey Chirwa
Shaban Chilunda
0 COMMENTS:
Post a Comment