ARSTICA Cioaba, Kocha Mkuu wa Azam FC ana kibarua kizito cha
kusaka pointi tisa za moto ndani ya mwezi Juni kutokana na hasira za wapinzani
wake kujipanga kulipa kisasi katika mechi tatu itakazocheza.
Azam FC ikiwa nafasi ya pili kibindoni imejikusanyia pointi 54
baada ya kucheza mechi 28 imebakiza mechi 10 ambazo ni dakika 900 kukamilisha
mzunguko wa pili.
Ofisa Habari wa Azam FC, Zaka Zakazi amesema kuwa mechi zao zitakuwa na ushindani kutokana na kujipanga kwa wapinzani wao
kulipa kisasi kutokana na balaa ambalo walilipata walipokutana.
“Tupo tayari kwa ligi na ushindani pia, ila mechi zetu zitakuwa
ni kali na za kisasi kutokana na wapinzani wetu kujipanga kulipa kisasi kwani
mechi zao zilizopita tuliwapa tabu hivyo watajipanga,” amesema.
Mechi tatu za
Azam FC zitakuwa namna hii:-Juni 14, dhidi ya Mbao, Uwanja wa Azam Complex.
Mechi ya kwanza Azam FC ilishinda bao 1-0. Juni 21, dhidi ya Yanga Uwanja
wa Taifa. Mechi ya kwanza Azam ilishinda bao 1-0 na Juni 24, dhidi ya
Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba mechi ya kwanza ziligawana pointi mojamoja.
0 COMMENTS:
Post a Comment