DITRAM
Nchimbi, mshambuliaji anayekipiga ndani ya Yanga amesema kuwa watawashangaza
wengi kwa kuonyesha kiwango ambacho hawatakiamini ndani ya uwanja.
Nchimbi amesema kuwa walikuwa nje kwa muda mrefu kutokana
na janga la Virusi vya Corona ambalo lilisimamisha masuala mengi ya michezo.
Hakukuwa na
mechi ya ushindani tangu Machi 17, tayari Serikali imeruhusu masuala ya michezo
kuanza na Yanga kwenye ligi itaanza na Mwadui FC, Juni 13 Uwanja wa Kambarage.
Nchimbi amesema kuwa wakati wa mapumziko alikuwa anafanya mazoezi kwa kuzingatia program aliyopewa na Kocha Mkuu, Luc Eymael na kuongeza zaidi.
“Nilikuwa ninafanya mazoezi nilipokuwa nyumbani kwa kuzingatia program ya mwalimu na wakati mwingine nilikuwa ninaongeza zaidi hivyo nina amini mashabiki hawataamini kile tutakachokifanya uwanjani kutokana na morali ambayo tunayo kwa sasa,” amesema.
Nchimbi ametupia mabao sita kwenye ligi na pasi mbili za mabao, alifunga mabao manne alipokuwa ndani ya Polisi Tanzania na Yanga ameifungia mabao mawili kati ya 31.
0 COMMENTS:
Post a Comment