UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa hauna mashaka na mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa kati ya Juni 27/28 Uwanja wa Taifa.
Mchezo huo wa hatua ya robo fainali umeshika hisia za wengi kutokana na ushindani wa timu hizi mbili kila zinapokutana uwanjani.
Mshindi wa mchezo huu atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Yanga ama Kagera Sugar kwenye hatua ya nusu fainali.
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin, amesema kuwa wapo tayari kupambana na mpinzani yoyote uwanjani kutokana na kuwa na kikosi imara.
"Ni ngumu kusema kwamba hatupo tayari ilihali kikosi chetu kipo vizuri na ni mabingwa watetezi, hatuna mashaka dakika 90 huwa hazidanganyi, tutapambana kupata matokeo wapinzani wetu tunawaheshimu ila hamna namna tunahitaji ushindi," amesema.
Azam FC ni mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho ambalo walilipata kwa kuitungua Lipuli FC bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa Lindi.
0 COMMENTS:
Post a Comment