June 4, 2020


MAJEMBE manne ya kazi yameruhusiwa kutua Yanga kukipiga msimu ujao iwapo mambo yatakwenda sawa.

Majembe hayo yanakipiga ndani ya Klabu ya Rayon Sports ya Rwanda ambao ni Michael Sarpong, Ally Niyonzima, Jules Ulimwengu na Fabrice Mugheni.

Nyota hao kwa sasa wanaweza kutua Bongo kwa kuwa Shirikisho la Soka Rwanda,(Ferwafa) limemaliza msimu mazima kwa kuipa ubingwa APR na kuwafanya wachezaji wanaomaliza mikataba kuwa huru kusepa.

Habari zinaeleza kuwa muda wowote wanaweza kuja kuongea na Yanga ila kitakachowachelewesha ni suala la mipaka ambayo bado imepigwa pini kutokana na kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.


 "Wanaweza kuja wakati wowote kwa kuwa Ligi Kuu ya Rwanda imefutwa, kitkachowazuia kuja mapema ni mipaka kufungwa ila mambo yakiwa sawa watakuja," ilieleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi na Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said amesema kuwa iwapo wanahitaji kumpata mchezaji hawawezi kushindwa.

8 COMMENTS:

  1. Hao ndio wale wa ligi tano Bora Africa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hawakumwelewa vizuri kwani Afrika Mashariki nayo si Afrika. bado Yanga wako sahihi simba tuendelee kuwaunga mkono tusiwalatishe tamaa jamaa zetu

      Delete
  2. Rwanda ipo kwenye ligi tano bora za Africa?

    ReplyDelete
  3. Wameshindwa kuchukua ligi ya Rwanda watatusaidia nini sisi ambayo ligi yetu ina ushindani zaidi?Pesa ndio mpira wa kisasa. Bila investment ya nguvu tutabaki tunapiga mark time.Tutaishia föda za magazetini.

    ReplyDelete
  4. halafu, hao wachezaji ndio kocha amewataka? au wa viongozi? Makambo kaaumia lakini yanga wanamtaka. akili mbovu kweli yanga

    ReplyDelete
  5. Shuka likiwa fupi lazima ukunje miguu.

    ReplyDelete
  6. Yote uongo!! Mtu pekee anayeweza kutua ni huyo kiungo!! Luc alishawaambia yeye ni mtaalam wa kudash Julia akapiga kushoto au mbele.

    ReplyDelete
  7. Yanga imepoteza dira mpira unachezwa mdomoni wakienda uwanjani hawana mpya wanabaki kujifariji kwa kuleta komedi za bingwa kabebwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic