MTENDAJI Mkuu wa Azam
Media, Tido Mhando, jana amezindua rasmi tamthilia nne ambazo zitarushwa kwenye
Chanel 103 ya Sinema zetu ukiwa ni mpango endelevu wa kuleta ushindani kwenye
masuala ya filamu kitaifa na kimataifa.
Uzinduzi huo
ulifanyika kwenye Ukumbi wa Hotel ya Kilimanjaro, ulihudhuriwa na waigizaji
wakongwe na chipukizi ambao walicheza kwenye tamthilia hizo.
Mhando alisema,
tamthilia hizo nne ni pamoja na Shilingi iliyozalishwa na kampuni ya
Omary Film Ltd na Tandi iliyozalishwa na kampuni ya JK Production ambazo
zitarushwa siku ya Ijumaa na Jumapili majira ya saa 3 usiku kuanzia Julai 17.
Panguso iliyozalishwa
na kampuni ya Wateule Inc na Single Mama iliyozalishwa na JB Film Company
zitaonyeshwa kuanzia Jumatatu mpaka Alhamisi, kuanzia Julai 13.
Mhando amesema:-"Tunarejea
upya na tulianza mpango huu kuupanga tangu mwishoni mwa mwaka 2019 na sasa kazi
imeanza.
" Malengo makubwa ya Azam TV ni kuona kwamba tunaweza kushindana na
wenzentu walioanza ikiwa ni wale wa Ghana na Nigeria na inawezekana kwa kuwa
nia ipo, na wote ambao tunafanya nao kazi ni wazawa wenye vipaji.”
0 COMMENTS:
Post a Comment