June 3, 2020




Daktari mkongwe wa michezo ambaye sasa ni daktari wa klabu ya Yanga, Shecky Mngazija amefichua kuwa winga wa kikosi hicho, Juma Mahadhi yupo fiti baada ya kupona majeraha yake lakini amekuwa muoga wa kucheza kutokana na kuhofia kuumia tena.

Mngazija ameongeza kwamba kwa sasa hakuna tatizo lolote kwa Mahadhi kuanza kutumika katika kikosi cha kwanza kwa sababu amepona na yupo fiti kabisa kupambana baada ya kukaa nje kwa zaidi ya msimu mzima.

Kwa muda mrefu Mahadhi amekuwa nje ya uwanja kutokana na kusumbuliwa na goti ambapo hivi karibuni alianza mazoezi ya pamoja na wachezaji wenzake katika Uwanja wa Chuo cha Sheria, Dar.

Mngazija amesema kuwa straika huyo kwa sasa anasumbuliwa na hofu ya kuwa anaweza kuumia baada ya kukaa sawa lakini hana tatizo lolote kutokana na kupona kabisa jeraha lake.

“Wale ambao walikuwa wakimtibu Mahadhi wametuhakikisha kabisa kwamba hana tatizo na wamempa ruhusa kabisa ya kuanza kucheza kwa mara nyingine.

“Tatizo lililopo kwake kwa sasa ni kuwa bado hajawa sawa kwani anaogopa kuwa anaweza kucheza na akaumia tena ingawa yupo fiti na anaweza kupambana kwa sababu waliokuwa wakimsimamia wametuhakikishia juu ya hali yake kwa asilimia zote,” alisema Mngazija.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic