SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kuna uwezekano wa kiungo wa Simba ambaye yupo Zambia Clatous Chama akaibuka Bongo, Juni 8.
Chama ni miongoni mwa wachezaji ambao walisepa Bongo baada ya ligi kusimamishwa kutokana na janga la Virusi vya Corona.
Tangu Machi 17 hakukuwa na mechi ya ushindani kutokana na Serikali kusimamisha masuala ya michezo kuchukua tahadhari ya Virusi vya Corona.
Tayari Simba imeshaanza mazoezi kujiandaa na mechi za ligi ambazo zinatarajiwa kuanza Juni 13 baada ya Serikali kuruhusu masuala ya michezo.
Jembe hilo la kazi limefunga mabao mawili na pasi saba za mabao huku Simba ikiwa imefunga mabao 63.
0 COMMENTS:
Post a Comment