June 24, 2020


INJINIA Hersi Said amesema kuwa mchezaji wa Yanga, Bernard Morrison amesaini kandarasi ya miaka miwili mbele ya macho yake hivyo ni mali halali ya Yanga kwa sasa.

Injinia Said ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji ndani ya Kampuni ya GSM ambao wanashiriki katika masuala ya usajili wa Yanga amesema kuwa hakuna mjadala kuhusu mkataba wa Morrison kwa kuwa ameshasaini kandarasi ya miaka miwili kinachotokea kwa sasa amepewa mkataba na timu nyingine.

Said ameongeza kuwa alifuatwa na Morrison akiomba kuvunja mkataba ili asajiliwe kwenye timu ambazo zimehitaji kupata saini yake ili asaini kwenye timu hizo.

"Morrison alinifuata aliniambia kwamba anaomba avunje mkataba wa miaka miwili ambayo alikuwa amesaini kwa kuwa amepata klabu ambayo inampango wa kumpa dili na itamlipa vizuri zaidi.

"Nilichomwambia mimi ni kwamba kama anahitaji kuvunja mkataba ni lazima utaratibu ufuatwe kwani yeye kwa sasa ni mali ya Yanga hivyo ni lazima klabu ambazo zinahitaji saini yake zizungumze na uongozi wa Yanga.

"Kinachomsumbua kwa sasa ni tamaa anahitaji kupata fedha nyingi baada ya kuona kwamba kuna timu nyingi zinamhitaji ila ukweli ni kwamba yeye ni mchezaji wa Yanga na mazungumzo ya yeye kuondoka ni lazima yafanyikwe kwenye timu," amesema. 

Leo gazeti la Championi Jumatano ambalo lipo mtaani limeandika kuwa Morrison ana mkataba wa miezi sita na ni mchezaji mwenyewe amesema.

Kuna mambo mengi amezungumza hali iliyopelekea apigwe faini na uongozi wa Yanga pia

15 COMMENTS:

  1. Sio filamu,pia uyo mchezaji hajielewi na tamaa zake zitamponza,pia nyinyi waandishi wa habari mnachangia kiasi kikubwa sana kuvuru kwasababu ya mapenzi yenu yatimu mnazozishabikia fanyeni kazi zenu kwa weledi acheni mapenzi yenu ya ovyo

    ReplyDelete
  2. Waandishi wa habari hawana makosa yoyote, kwani kwao wakisikia tetesi lazima wazifanyie kazi bila kujali zinatoka wapi. Suala la Morisson lazima lihojiwe pande zote. Mchezaji anaposema hana mkataba zaidi ya ule unaokoma mwezi Julai wakati klabu inatangaza kwamba ana mkataba mwingine, lazima tujiulize kuna nini hapo?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Msimwamini sana Morrison alishashitakiwa Afrika ya Kusini kwa utapeli...wachezaji wa Afrika Magharibi wanafahamika kwa ulaghai na tamaa ya fedha na uongouongo

      Delete
  3. Yamekuwa hayo. Kwani mlikuwa hamjui kwamba ametoka Afrika Magharibi?Wekeni mkataba hadharani wacheni maneno.

    ReplyDelete
  4. Na hado, mlimtukuza kupita kiasi akavimba kichwa

    ReplyDelete
  5. Walikuwa wanamsifia anapanda mpira, sasa anawapanda wao vichwani

    ReplyDelete
  6. Tuwe wakweii, GSM wanawasainisha wachezaji wakachezee timu ipi kwani kuna GSM sports club? Kama na wafadhali watoe mpunga viongozi halali wa yanga ndio waingie mikataba na wachezaji, vinginevyo kila kitu ni batili

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha usenge wewe angalia kwenye mkataba wake kama kuna sahihi ya mtu wa GSM?Mnakurupuka kama mikia fc!

      Delete
  7. Engineer Hersi said umeeleweka vizuri sana

    ReplyDelete
  8. Acha lugha za kuudhi, usenge ndio nini kama sio mchezo wako wewe?

    ReplyDelete
  9. Enter your comment...asitumie nguvu nyingi, yeye kama mkataba wake miezi 6 asaini tu timu nyingine. hamna haja ya kuzungumza na vyombo vya habari

    ReplyDelete
  10. iyo inaitwa mnyongaji kanyongwa poleni sana watani yanga, katika maisha pesa na muda ni vitu viwili vinaenda kasi sana GSM ni mdhamini tu wa timu yenu, kumbukeni kuna kiongozi apo siku za nyuma alisema kama kweli GSM anatowa pesa angetowa pesa kwa uwongozi wa timu then viongozi wafanye usajili wao watimu yule jamaa aliposema GSM wakaja juu wakadai wanajitowa kuidhamini yanga mashabiki wa yanga mkaandamana mbaka kwenye makao makuu ya timu pale jangwani mkapiga kelele kuwa uwongozi unataka kuujumu timu haiwezekani GSM ajitowe, yule kiongozi akaambiwa ajiuzulu waka jiuzulu wengi tu viongozi, kiongozi wa mwisho alisema kuwa morisoni ajasaini mkataba yanga GSM wakaja juu wakadai yule kiongozi ana waujumu ametowa siri ya ndani ya timu kwa hiyo ajiuzulu bac jamaa akaona isiwe tabuu sana akajiuzulu wakati Alisha sema ukweli aikupita ata siku 5 morisoni akagoma akaja na stori Simba wananitaka wamemtuma wakala wao kaja kanipa dollars 5000, juzi akaja yeye mwenyewe morisoni time hii kaja kivingine kabisa kaweka kila kitu wazi kuwa yeye mkataba wake na yanga unaisha mwezi wa 7, swali lina kuja kati ya yanga na morisoni ni nani mkweli na kama yanga wao wanadai jamaa amesaini miaka 2 c watowe mkataba wazi ili kila mwanayanga ajuwe ukweli ila kinacho onekane apa viongozi wa yanga walijuwa labda uwenda tabia ya morisoni ni sawa na tabia ya mrisho ngasa, mrisho ngasa yeye ana mapenzi na yanga ila morisoni amekuja kutafuta pesa na si mapenzi na timu ndo maana ameamuwa kuweka mambo wazi ili kila mwenye akili ajuwe sasa mmekamatika yanga poleni sana, morisoni kawa panda vichwani badala ya kupanda mpira⚽⚽. 🤣🤣🤣

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic