INJINIA, Hersi Said amesema kuwa GSM imejipanga kwa ajili ya kuboresha kikosi cha Yanga hivyo hawashindwi kumpata mchezaji yeyote ndani ya ardhi ya Tanzania.
Miongoni mwa wachezaji ambao inaelezwa kuwa Yanga inapambana kupata saini yake ni pamoja na beki chipukizi wa Coastal Union, Bakari Mwamnyeto ambaye inaelezwa kuwa amemalizana na Simba baada ya Yanga kushindwa kumpa dau alikuwa analihitaji.
Kauli hiyo ya kibabe ni kama mkwara wa kimtindo kwa watani zao wa jadi Simba ambao inaelezwa wapo kwenye harakati za kuiwinda saini ya beki huyo ambaye pia ni nahodha.
Said amesema:"Mchezaji yeyote ndani ya Tanzania ambaye tunaona yupo kwenye viwango vyetu tunavyovitaka ili kuitumikia Yanga hatuwezi kumkosa kupata saini yake.
"Malengo yetu makubwa ni kuona kwamba Yanga inakuwa imara na inaweza kuwa kwenye ushindani kitaifa na kimataifa," amesema.
Ndizi mbichi hizi. Poleni GONGOWAZI mmeshindwa dau hamna pesa hata kocha hamjamtumia tiketi hadi leo GONGOWAZI
ReplyDelete