MTIBWA Sugar iliyo chini ya Kocha Mkuu, Zuber Katwila ikiwa imecheza jumla ya mechi 32 kibindoni ina pointi 37.
Safu yake ya ulinzi inayoongozwa na kinda Dickson Job imeruhusu jumla ya mabao 29 ya kufungwa.
Safu ya ushambuliaji imetupia jumla ya mabao 25 na katika mabao hayo kiungo wao Abdulrahman Humud ametupia mabao mawili.
Haikuanza msimu vizuri kutokana na ushindani ambao ilikuwa inakutana nao hasa baada ya kushinda Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar.
Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobisa Kifaru amesema kuwa baada ya kushinda taji hilo kwa kuitungua Simba bao 1-0 wapinzani wao walikuwa wanawakamia.
Kibarua chake kwa sasa ni kuweza kutetea nafasi yake ndani ya Ligi Kuu Bara kutokana na nafasi ambayo ipo kwa sasa kutokuwa salama.
Katwila anaamini kwamba vijana wake wanaweza kurejea kwenye ubora taratibu na kuanza kupata matokeo chanya kwenye mechi zao zilizobaki.
0 COMMENTS:
Post a Comment