ARISTICA Cioaba, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa hesabu zake kubwa kwa sasa ni kwenye mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbao FC utakaochezwa Juni 14, Uwanja wa Azam Complex.
Cioaba raia wa Romania, jana alitesti mitambo ya kikosi chake kwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Transit Camp na kuambulia sare ya bila kufungana ndani ya dakika tisini.
Matokeo hayo hayajamkasirisha Mromania huyo na badala yake amesema kuwa ni sehemu ya mchezo kwa kuwa wachezaji wake hawakuwa na mechi ya ushindani kwa muda mrefu.
Tangu Machi 17 hakukuwa na mechi ya ushindani iliyochezwa Bongo kutokana na Serikali kusimamisha masuala ya michezo ili kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona na kwa sasa tayari Serikali imeruhusu masuala ya michezo kuendelea kwa kueleza kuwa maambukizi yameanza kupungua.
"Wachezaji hawakuwa na mechi ya ushindani kwa muda mrefu hivyo kwa matokeo ambayo wameyapata sio mbaya. Makosa ambayo nimeyaona tutayafanyia kazi kwenye mchezo ujao," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment