MASTAA 29 wa Klabu ya Yanga ambao wameanza mazoezi hivi Mei 27 katika chuo cha Sheria walimnyima Kocha Msaidizi, Charlse Mkwasa kiasi cha sh.290,000,(laki mbili na elfu tisini)
Yanga imeanza mazoezi ya pamoja Mei 27 kwa ajili ya kujiweka sawa na mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe za Shirikisho.
Picha lipo namna hii, kabla ya kuanza mazoezi hivi karibuni, Mkwasa aliwaambia wachezaji wake kuwa yeyote atakayeangusha mojawapo ya vikwazo (Cone) atakatwa 10,000.
Jambo hilo liliwafanya wachezaji kupambana kufanya vema na licha ya kufanya zoezi hilo zaidi ya mara moja hakuna aliyedondosha kikwazo hicho.
Kwa hesabu hizo, wachezaji 29 walipambania sh.10,000 zao hivyo Mkwasa kushindwa kuambulia chochote.
Wafikishie Ujumbe Yanga
ReplyDeleteKwanini mpaka sasa hawajawaleta na kukamilisha idadi ya benchi lao la Ufundi? Safari za ndege zimefunguliwa siku nyingi Ulaya na sehemu nyingine lakini makocha wa Yanga bado hawajawasili hili ni doa...na wana siku 10 tu kabla ya kuanza kwa ligi daktari na Wachua misuli Kocha wa fitness na kocha mkuu wote wanatokea nje ya nchi lakini bado hawajaripoti kambini...wakati Azam Kocha wao wamemfanyia njia ya haraka na sasa amewasili na anaendelea na program....Yanga yale madudu na virusi vinavyorudisha nyuma maendeleo bado vipo? Tafadhali sana hili lirekebishwe!
Sio kila nchi imefungua mipaka yake.......
Delete