IDADI kubwa
ya mashabiki wamezoea kuona katika mechi mwamuzi wa mezani akiongeza dakika
mbili, tatu au nne lakini zinapoongezwa zaidi ya hizo basi kunaibuka minong’ono
ya hali ya juu.
Zipo sababu
nyingi zinazochangia mwamuzi kuongeza idadi kubwa ya dakika kabla ya mechi
kuisha miongoni mwao ni pamoja na kama timu moja ilipoteza muda, tukio la
kuumia wachezaji au mechi kusimama kutokana na majanga ya kiasili.
Kuna idadi
nyingi tu ya mechi ambazo zimewahi kuongezwa zaidi ya dakika tano kabla ya
kumalizika. Jambo hilo limejitokeza katika Ligi Kuu Bara ambapo kuna mechi
ziliongezwa zaidi ya dakika tano.
Katika
makala haya kuna mechi za Ligi Kuu Bara ambayo ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 13 baada ya masuala ya michezo kusimama kutokana na janga la Virui vya Corona hizi hapa :-
Azam vs Kagera Sugar dk 9
Hii ndiyo
mechi ambayo hadi sasa inashika rekodi ya kuwa mechi iliyoongezwa muda mrefu
baada ya ule wa awali yaani dakika 90 kumalizika. Mechi hii ilipigwa Uwanja wa
Azam Complex na kumalizika kwa suluhu.
Kwenye mechi
hii ziliongezwa dakika tisa baada ya zile 90 kugota ukingoni lakini licha ya
muda wote huo ambao uliongezwa timu hizi hazikufungana na kugawana pointi moja.
Pambano hili lilipigwa Novemba 4.
Simba vs Prisons dk 7
Katika
mchezo huu kwa mara ya kwanza Simba wakai ule ikiwa chini ya Mbelgiji wake Patrick Aussems
walipata sare kwenye mechi zao za ligi baada ya kucheza mechi saba wakishinda
sita na kufungwa moja.
Katika
mchezo huu ziliongezwa dakika saba baada ya zile 90 kumalizika kitu ambacho
kiligeuka gumzo katika mitandao mbalimbali wengi wakijadili juu ya kuongezwa
kwa dakika hizo. Hata hivyo licha ya dakika saba kuongezwa mwishoni walitoka
suluhu.
Mtibwa vs Polisi Tanzania dk 6
Ingawa
Mtibwa Sugar walianza kwa kupepesuka katika ligi lakini walipokutana na Polisi
Tanzania waliamka na kuwachapa mabao 2-0 katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Sasa weka kando ishu hiyo ya matokeo kitu kikubwa kilichojitokeza ni ishu ya
kuongezwa kwa dakika nyingi baada ya zile 90.
Mechi hii
ilishuhudia dakika sita zikiongezwa kabla ya kumalizika kwake lakini dakika
hizo hazikuwa na faida yoyote kwa Polisi kwani mwisho waliziacha pointi tatu
katika uwanja huo.
Mbao vs Tanzania Prisons dk 6
Miongoni mwa
mechi ambazo zilipigwa hadi jioni sana kwenye Ligi Kuu Bara kwa msimu huu ni
hii ikichezwa kwa dakika 90+6, ambapo ilipigwa katika Uwanja wa CCM Kirumba
mkoani Mwanza na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Alliance vs Mbeya City dk 5
Shughuli
nzima ilifanyika katika Uwanja wa Nyamagana, Mwanza ambapo mchezo huu ulikuwa
na matukio kwelikweli. Kumbuka hii ndiyo mechi ambayo wachezaji wawili wa
Alliance walikula ‘umeme’ kwa vitendo visivyo vya kiuanamichezo akiwemo kipa wa
timu hiyo jambo ambalo lilisababisha beki Siraji Juma kukaa langoni.
Sasa sahau
kabisa ishu hizo kitu kingine kilichokuwa gumzo ni dakika tano ambazo
ziliongezwa ambapo kwa Alliance ambao walikuwa nane uwanjani zilikuwa nyingi na
Mbeya City ambao walikuwa 11 walishindwa kuwafunga wapinzani wao wakiwa
pungufu.
Yanga vs Ruvu Shooting dk 5
Ukiwa mchezo
wa kwanza tu kwa timu zote. Yanga walijikuta wakiangukia pua kwa kufungwa bao
1-0 na maafande hao, ambapo huu ulikuwa mchezo wa kwanza kwa Kocha Mwinyi
Zahera aliyekuwa Yanga kupoteza katika msimu.
Mzigo huu ulipigwa
Agosti 28, katika Dimba la Uhuru na mechi hii iliingia kwenye rekodi za
kuchezwa kwa muda mrefu msimu huu kwa kuongezwa dakika tano.
Yanga vs Polisi Tanzania dk 5
Wengi
wanaikumbuka mechi hii kwani ndiyo ilimpaisha Ditram Nchimbi baada ya kufunga
hat trick. Mechi hii licha ya kuwa kali na kusisimua iliingia kwenye rekodi ya
kuchezwa kwa muda mrefu baada ya kupigwa kwa dakika 95 yaani 90 za kawaida na
zile tano za nyongeza.
0 COMMENTS:
Post a Comment