MECKY Maxime, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa wanajiadaa kutoa burudani kwenye mchezo wao wa hatua ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa kati ya Juni 27 na 28 Uwanja wa Taifa.
Akizungumza na Saleh Jembe, Maxime amesema kuwa walikosa kutoa burudani kwa muda mrefu kutokana na janga la Virusi vya Corona hivyo wanajipanga kufanya vizuri.
“Tutakuwa na mechi za ligi kabla ya kucheza na Yanga hivyo maandalizi siku zote huwa hayabadiliki, nina amini kwamba tutatoa burudani kwenye mchezo wetu dhidi ya Yanga kwani tunahitaji ushindi,” amesema.
Kagera Sugar ilitinga hatua ya robo fainali kwa kuanza kumenyana na Rufiji United na kuitoa kwa mabao 4-1 kisha ikapenya mbele ya Might Elephant mzunguko wa 32 kwa kushinda 2-0 na hatua ya 16 mbele ya KMC ilishinda kwa penalti 2-0 baada ya dakika 90 kukamilika kwa kufungana bao 1-1 mechi zote zilichezwa Uwanja wa Kaitaba.
0 COMMENTS:
Post a Comment