June 1, 2020


ANAANDIKA Saleh Jembe kuhusu maoni masuala ya nembe ndani ya Klabu ya Yanga namna hii:-Nimezungumza mara nyingi sana kuhusiana na hili suala lakini WASIO NA HOJA akaishia kwenye Matusi, sasa leo TUJIFUNZE TENA.

ANGALIA LOGO ya Sevilla FC ina rangi nyingi nyekundu na leo Yanga wanaingia nao mkataba logo yao ikiwa na rangi zake.

Hapa nyumbani kampuni zote zilizoingia mkataba na Yanga kwa maana ya kuwa zinatoa fedha, bado Yanga walishindwa kuonyesha heshima na baadaye kulazimika kubadili rangi za logo zao.


 Mfano mzuri, wadhamini wa ligi Vodacom ambao Yanga wanafaidika nao... Angalia GSM PIA.

Utasikia sisi hatuwezi kufanya kazi na watu wenye rangi nyekundu.

Nimefafanua mara nyingi sana kuwa si kila nyekundu ni Simba au kila njano ni Yanga.

Wadhamini au partners wanapaswa KUHESHIMIWA na vizuri tukaacha "USHAMBA WA RANGI"... Hili la  Sevilla na La Liga linaweza kuwa funzo kwa wale ambao kweli hawakuwa wakielewa au wale walikuwa HAWAELEWI KWA MAKUSUDI..

9 COMMENTS:

  1. Hueleweki umeandika nini,Yanga wanapinga kueka rangi nyekundu kwenye jezi yao na sio kushirikiana na timu au kampuni yenye rangi nyekundu,Ushirikiano wa sevilla na Yanga c ushirikiano wa kuifanya Yanga waiweke kwenye Jezi yao Logo ya Sevilla..fikiri kwanza kabla ya kuandika

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyu mwandishi ni mbabaishaji siku zote. Ushabiki wake wa Simba unamfanya akose weledi daima!

      Delete
  2. Muandishi ameteleza, inaonekana hajafanya uchambuzi wa kina.
    Nivyema habari iwiyane na sababu gani zinapelekea kupinga rangi hizo na wakati gani? ...

    ReplyDelete
  3. Yanga bado 🐥 🐥 tu xo itawachukuwa muda xana na yote ni uxhamba tu wao Wana amini rangi nyekundu ni simba, ata nembo ya voda com ambae ni mdhamini wa ligi kuu Tanzania bara ni nyekundu xo walipiga kelele xana yanga viongozi mbaka maxhabiki wao ila yote ni kutojielewa hawa bado fikra zao zipo miaka ya 1775 mbaka kizazi hiki nacho wanatembelea kivuli hicho hicho xo acha watoe povu tu ila ukweli wameupata.

    ReplyDelete
  4. Salehe usimba unakusumbua, Yanga wanachokataa ni kuweka logo nyekundu kwenye jezi zao na sio kuingia mkataba wa ushirikiano. Yanga wanashirikiana na kampuni nyingi tu zinazotumi rangi nyekundu ila sio kuweka kwenye jezi. Ni aibu mmeshindwa kukosoa mkataba sasa mnahangaika na vitu vidogo kama logo, what a shame

    ReplyDelete
  5. Wewe ndio mshamba kuliko maana unajifanya kuelewa wakati huelewi, Yanga wanachokataa ni kuweka rangi nyekundu kwenye jezi zao!

    ReplyDelete
  6. yanga wanatembea kikale kale, rangi rangi wataendelea kubaki nyuma mnyama huyooo anasepa kimataifa

    ReplyDelete
  7. kaka mkubwa, mihemuko ya Usimba inakupa tabu sana, ungefikiri kabla ya kuandika. pole sana sana. unazidi poteza credibility yako kwa ukurupujaji

    ReplyDelete
  8. Kabla ya kuandika huo uharo wako ungejiuliza nembo ya GSM ina rangi gani?na sio kukurupuka tu na kutafuta penseli ukaanza kuchora chora kwenye karatasi na kisha ukatupia hapa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic