LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga ameamua kuvunja ukimya na kuweka wazi juu ya hatma ya winga wa kikosi hicho, Mghana, Bernard Morrison, ambaye amekuwa akihusishwa kujiunga na Simba.
Ikumbukwe kuwa, tangu Machi, mwaka huu kulikuwa na taarifa zilizokuwa zikimhusisha Morrison kujiunga na Simba, wiki iliyopita kupitia mitandao ya kijamii, Morrison alisikika akidai kuwa alipewa dola 5000 (milioni 11, 560, 000), ikiwa kama sehemu ya kumshawishi atue Simba.
Eymael amesema Morrison hawezi kwenda Simba kwa sababu tayari ameshasaini Yanga na kama ikitokea akasaini Simba basi atafungiwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), kwa muda wa miaka miwili.
“Unajua Morrison tayari ameshasaini Yanga, hawezi tena kwenda Simba, kama ikitokea akasaini Simba, basi ni lazima atafungiwa na FIFA, kwa muda wa miaka miwili kama ambavyo sheria inasema,” amesema Eymael.
Morrison amecheza mechi 10 za ligi na kuhusika kwenye mabao sita kati ya 32 yaliyofungwa na yanga, akifunga matatu na kutoa pasi tatu.
Ikiwa ni kweli Simba wametowa hela kuchota Morrison basi Simba sio wajing na wanazijuwa Sheria zote. Kama hamna la kusema ni bora kunyanaza, lakini msiwatishe wenye akili
ReplyDeleteHao jamaa imewajaa hofu na wanajaribu kumtisha Morrison. Simba wanakanusha kumtaka Morisson lakini juu ya hivo, Vipi aadhibiwe na dirisha la usajili bado halijafunguliwa. Jamaa wanaviogopa hata vivuli. Wao si wanawataka wachezaji wa Simba kibao mbona hapana wanaotowa vitisho kila kukicha na huku wakimtaka Chama wakijuwa Ana mkataba na Simba
ReplyDeleteSuala sio ujinga suala Ni tamaa, marangapi hata vilabu vikubwa vya ulaya vinakosea na kupigwa faini, inamaana havijui sheria? Inawezekana Simba wanafanyahivyo ili kuwapunguzia Yanga nguvu, kwasababu hata akifungiwa kwao sio issue.
ReplyDeletePoint mzee baba
DeleteKila timu inafahamu Sheria za usajili yetu macho
ReplyDelete