June 24, 2020


AZAM FC leo ina kazi ya kumenyana na Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa majira ya saa 10:00 jioni Uwanja wa Kaitaba.

Azam FC liyo chini a Kocha Mkuu, Aristica Cioaba ina kibarua kizito cha kumenyana na Kagera Sugar iliyo chini ya Kocha Mkuu, Mecky Maxime.

Kwenye mchezo wao wa kwanza walipokutana Uwanja wa Chamazi, Kagera Sugar iliambulia pointi moja kwa sare ya bila kufungana na Azam FC.

Mchezo wao uliopita Azam FC ililazimisha sare ya bila kufungana na Yanga Uwanja wa Taifa huku Kagera Sugar ikipoteza kwa kufungwa mabao 2-0.

Azam FC inapambana kulinda nafasi yake ya pili ambapo ikiwa imecheza mechi 30 kibindoni ina pointi 58 na Kagera Sugar ikiwa imecheza mechi 30 ipo nafasi ya 9 ikiwa na pointi 41.

Vita kubwa kwa sasa kwa timu hizi zote mbili ni kwa upande wa nafasi Azam ikiwa inasaka nafasi ya pili, Kagera Sugar inataka kubaki ndani ya 10. 

Mtupiaji namba moja ndani ya Azam FC ni Obrey Chirwa kibindoni ana mabao nane huku Kagera Sugar namba moja wao ni Yusuph Mhilu mwenye mabao 11.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic