June 24, 2020


LEO saa moja kamili Usiku, Uwanja wa Taifa kutakuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga na Namungo FC. 

Mchezo huu wa Ligi Kuu Bara ikiwa ni mzunguko wa pili unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili.

Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael mkali wao wa kucheka na nyavu ni David Molinga akiwa na mabao nane huku kwa Namungo mtupiaji wao namba moja ni Relliants Lusajo mwenye mabao 12.

Kuwaona nyota wa Yanga wakimenyana na Namungo, ikiwa ni pamoja na Bernard Morrison mwenye mabao matatu huku kwa Namungo akiwa ni Lukas Kikoti mwenye mabao manne kiingilio cha chini kabisa ni buku tano (5,000) kwa viti vya mzunguko.

 VIP A 15,000 , B&C 10,000 na mzunguko 5,000 huku kwa yule atakayenunua jezi ya Yanga kwa shilingi 20,000 atapewa tiketi bure ya mzunguko na jarida pia.


2 COMMENTS:

  1. Timu itakayowavuta mashabiki kwenda kuitaxama ni Namungo na si Yanga japo watakuwa wanacheza wote. Yanga ni butua butua tu wakiongozwa na Yirkpe walioshamchoka

    ReplyDelete
  2. Buku tano kwaajili ya kumuona Morison au kuona kichapo? Haki ya Mungu mumeishiwa ya kusema

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic