MANCHESTER United, imesema kuwa haipo tayari kutoa dau la zaidi ya paundi milioni 50 kupata saini ya Jadon Sancho anayekipiga ndani ya Borussia Dortmund.
Klabu yake ya Ujerumani inahitaji dau la paundi milioni 100 ili wamuachie nyota huyo raia wa England mwenye miaka 20.
Licha ya United iliyo chini ya Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solskjaer kuitaka saini yake yupo tayari kumkosa nyota huyo kwa msimu ujao iwapo dau lake halitapungua.
Nyota huyo anayevaa jezi namba saba mgongoni alijiunga na Dortmund msimu wa 2017 akitokea Klabu ya Manchester City amecheza jumla ya mechi 78 na kutupia mabao 30.
Kwa msimu huu amefunga jumla ya mabao 20 na kutoa pasi 19 kwenye jumla ya mashindano yote msimu huu.

0 COMMENTS:
Post a Comment