HARUNA Niyonzima,
kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa wana imani ya kuibuka na ushindi
mbele ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa, leo, Julai 30,
Uwanja wa Taifa.
Mchezo huo
unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa Yanga ilipoteza mchezo wa kwanza
wa Kocha Mkuu, Luc Eymael kwa kuchapwa mabao 3-0 na Kagera Sugar, Januari 15, Uwanja wa
Uhuru kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Akizungumza
na Spoti Xtra, Niyonzima ambaye alifunga bao lililoipa nafasi Yanga kushiriki
hatua ya robo fainali mbele ya Gwambina FC, alisema kuwa wapo tayari kwa
ushindani.
“Ukizungumzia
mchezo wa ligi ambao tulipotezwa ni tofauti na tutakavyokutana na Kagera Sugar
kwenye Kombe la Shirikisho, huku kwenye ligi tuna hesabu zetu tunakamilisha ila
huku kwenye FA lazima tupambane ili tuchukue kombe.
“Walitufunga
hatukatai ila wasitarajie wataweza kutufunga tena tutakapokutana, makosa ambayo
tuliyafanya tumeyafanyia kazi na tutapambana,” alisema Niyonzima.
Mshindi wa
mchezo wa Yanga na Kagera Sugar atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Simba na
Azam FC hatua ya nusu fainali.
0 COMMENTS:
Post a Comment