June 19, 2020


TUMEANZA kushuhudia ile burudani ambayo ilikuwa imekosekana kwa muda mrefu kwenye ulimwengu wa macho ya wanamichezo.
Nazungumzia mpira wa ushindani ambao umekuwa ukiwakusanya ndugu jamaa na marafiki sehemu moja huku kila mmoja akiwa na kile ambacho anakiamini kwa timu yake.
Ikumbukwe kuwa tangu Machi 17 hakukuwa na mechi ya ushindani ambayo iliweza kuonekana kwenye macho ya wanafamilia ya michezo.
Sababu kubwa ya yote hayo ni kutokea kwa janga la Virusi vya Corona ambalo kiukweli lilivurugavuruga vichwa vya wataalamu na kuisumbua dunia kiujumla.
Kwa kulitambua hilo Serikali iliamua kusitisha masuala ya michezo kwa lengo la kuchukua tahadhari. Kwa sasa Serikali imeridhia masuala ya michezo kuanza.
Juni 13 mambo yalikuwa ni mwendelezo wa palepale tulipoishia ambapo Mwadui FC wao walipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na Yanga Uwanja wa Kambarage kisha Coastal Union wao walipindua meza na kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 na Namungo.
Simba ilikubali sare ya kufungana bao 1-1 ilikuwa mbele ya Ruvu Shooting,Uwanja wa Taifa,ilikuwa ni bonge moja ya mechi.

Juni 17, JKT Tanzania 1-1 Yanga Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Moja ya matokeo ambayo yameushangaza ulimwengu wa soka ni pamoja na haya ya Namungo, ile kufumba na kufumbua ubao kipindi cha pili unabadilika.
Jambo jema ni kwamba Hitimana Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo amekubali matokeo na ameweka wazi kuwa wachezaji wake walishindwa kulinda ushindi ambao waliupata kipindi cha kwanza.
Ipo namna hii mabao ya Namungo yote mawili yalipatikana kipindi cha kwanza na walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao mawili.
Upepo ulibadilika kipndi cha pili ambapo mabao yote mawili yalirudhishwa na kufanya ngoma iwe 2-2. Huu ni ushindani ambao tulikuwa tumeokosa kwa muda mrefu na kila mmoja anapaswa apambane kuonyesha kwamba ana nia ya matokeo.
Ushindi ndani ya mpira upo kwenye maandalizi makini. Thiery ameweka wazi kwamba vijana wake walijisahau na kuamini kwamba mchezo umekwishwa.
Kwa makocha wa timu nyingine inaonyesha wamekuwa mafundi wa kutafuta sababu pale wanaposhindwa huku wakisahau kwamba kila timu inahitaji ushindi ni mfano mzuri Thiery umeonyesha katika hilo nakupa tano.
Ukiachana na Namungo ambayo imeanza msimu wake wa kwanza vizuri hapa kuna Singida United iliyo chini ya Kocha Mkuu, Ramadhani Nswanzurimo hapa kuna shida kidogo kutokana na ushindani uliopo.
Kwa wakati huu ambao umebaki ni muhimu kwa Singida United kufanya tathimini mara mbili na kujiuliza ni namna gani wanaweza kutenda miujiza ili wabaki ndani ya ligi.
Kuwa na pointi 15 baada ya kucheza mechi 29 ni pigo kubwa ambalo kujitoa hapo inahitaji akili na juhudi isiyo ya kawaida.
Ikumbukwe kuwa ni timu nne zinashuka mazima huku mbili zile za nafasi ya 15 na 16 play off ikiwahusu. Kila timu inakazi ya kujifunga mkanda ili kutetea nafasi yake itakayozubaa Daraja la Kwanza lipo mlangoni linagonga hodi.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic