SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa iwapo ataulizwa kwa sasa kama anaweza kuruhusu timu yake kurejea uwanjani hatakubali kwa kuwa wachezaji wake hawajawa na utimamu wa mwili.
Simba imeripoti kambini Mei 27 na kuanza mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na zile za Kombe la Shirikisho.
Ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 71 baada ya kucheza mechi 28 kibindoni imetupia mabao 63.
Kuhusu kurejea kwa ligi Sven amesema“ Ukiniambia kuwa kwa sasa tupo tayari kucheza nitakwambia hapana, sababu wachezaji hawana utimamu wa mwili.
" Kwa hizi wiki mbili zilizobaki kabla ya ligi kurejea zitatusaidia kutuweka vizuri.Tayari nimewaanzishia wachezaji program ya mazoezi ambayo itawarudisha taratibu kwenye ubora wao."
Juni 13 ligi kuu Bara inaanza kutimua vumbi baada ya Serikali kuruhusu kuanza kwa masuala ya michezo iliyosimamishwa tangu Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona.
Wafikishie Ujumbe Yanga
ReplyDeleteKwanini mpaka sasa hawajawaleta na kukamilisha idadi ya benchi lao la Ufundi? Safari za ndege zimefunguliwa siku nyingi Ulaya na sehemu nyingine lakini makocha wa Yanga bado hawajawasili hili ni doa...na wana siku 10 tu kabla ya kuanza kwa ligi daktari na Wachua misuli Kocha wa fitness na kocha mkuu wote wanatokea nje ya nchi lakini bado hawajaripoti kambini...wakati Azam Kocha wao wamemfanyia njia ya haraka na sasa amewasili na anaendelea na program....Yanga yale madudu na virusi vinavyorudisha nyuma maendeleo bado vipo? Tafadhali sana hili lirekebishwe!