June 18, 2020


ERASTO Nyoni, beki kiraka wa Simba amesema kuwa kupoteza pointi mbili mbele ya Ruvu Shooting hakujawatoa kwenye reli kwa kuwa wanaamini kuwa watapata matokeo chanya mbele ya Mwadui FC, Juni 20 Uwanja wa Taifa.
Nyoni alikuwa kwenye safu ya ulinzi wakati Simba ikitoka kwa sare ya kufungana bao 1-1, Juni 14 Uwanja wa Taifa ambapo bao la Simba lilifungwa na Shiza Kichuya na lile la Ruvu Shooting likifungwa na Fully Maganga.
Akizungumza na Spoti Xtra, Nyoni alisema kuwa hesabu kubwa zilizopo kwa wachezaji ni kupata ushindi kwenye mechi zao zilizobaki ili kutwaa Kombe la Ligi Kuu Bara.
“Mchezo uliopita matokeo yake hatuwezi kuyabadili tunachokifanya kwa sasa ni kutazama mipango yetu ya mbele, bado hatujatoka kwenye ramani kwani mipango yetu ni kushinda mechi zinazofuata ikiwa ni pamoja na ile dhidi ya Mwadui.
“Mashabiki wasikate tamaa kupata sare sio mwisho wa maisha ni lazima tuendelee kupambana ili kupata matokeo inawezekana kwa kuwa uwezo tunao tutafanya vizuri,” alisema.
Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 72 baada ya kucheza mechi 29, mchezo uliopita walipokutana na Mwadui FC ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Kambarage.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic